JERUSALEM: Maandamano yanukia huko Gaza
1 Agosti 2005Matangazo
Wakaazi wa kiyahudi wamesema wataendelea mbele na maandamano yao kuupinga mpango wa kuyaondoa makazi ya walowezi wa kiyahudi kutoka mkanda wa Gaza, hata licha ya maandamano yao kupigwa marufuku.
Shaul Goldstein, anayewaongoza wakaazi hao amesema wayahudi wasiopungua elfu 20 wanatarajiwa kukusanyika katika mji wa kusini wa Sderot hapo kesho, kabla kwenda kwenye makazi ya Gush Katif siku ya Alhamisi.
Waziri mkuu wa Israel, Ariel Sharon amewataka wayahudi watakaohamishwa kujaza fomu za malipo wiki mbili kabla mpango huo kuanza.