JEDDAH: Polisi wapambana na wanamgambo
13 Machi 2005Matangazo
Watu wawili wameuawa baada ya vikosi vya usalama vya Saudia Arabia kufyetuliana risasi na watu walioshukiwa kuwa wanamgambo mjini Jeddah.Maafisa wa Saudi Arabia wamesema askari polisi watano walijeruhiwa baada ya kuivamia fleti ya watu walioshukiwa kuwa ni wanamgambo,kaskazini mwa Jeddah.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani,raia mmoja wa kike pia ameuawa.Mtu mwengine amekamatwa kwa mashtaka yanayohusika na usalama.Uvamizi huo umetokea baada ya ubalozi wa Marekani nchini Saudi Arabia kutoa onyo jumanne iliyopita kuwa kitisho cha ugaidi kimezidi katika mji wa Jeddah.Miezi mitatu iliyopita wanamgambo waliokuwa na uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda, waliushambulia ubalozi mdogo wa Marekani nchini Saudi Arabia.