Nchini Tunisia maamuzi ya kujilimbikizia madaraka yanayoendelea kuchukuliwa na rais wa nchi hiyo Kais Saed yanazidi kuwatia mashaka wananchi wa taifa hilo la kaskazini mwa Afrika. Siku ya Jumapili, Rais Saed alipitisha amri ya kujipa mamlaka mengine ya kutimua majaji na kuzuia hatua ya kuwaongeza vyeo watumishi hao wa mahakama. Je nini hasa dhamira ya rais Kais Said?
Wanasheria nchini humo wanasema anachokifanya rais ni kinyume na katiba na kuondowa kabisa uhuru wa mahakama. Je nini hasa dhamira ya rais Kais Said kupitia hatua hizi? Tunisia inarudi kwenye utawala wa kiimla. Saumu Mwasimba amezungumza na mchambuzi wa kisiasa kutoka Tehran AbdulFatah Musa na kwanza anatoa mtazamo wake wa kinachoendelea hivi sasa Tunisia. Sikiliza!