Je, Taliban bado imetengwa baada ya miaka 4 uongozini?
20 Agosti 2025Mnamo mwezi Agosti mwaka 2021, serikali huko Afghanistan ilianguka na hivyo kutoa nafasi kwa Taliban baada ya Amerika kuondoa vikosi vyake kutoka Afghanistan.
Miaka minne baadaye, kundi la Taliban linaonekana kushikilia Madaraka kwa uthabiti na uimara kiasi cha kwamba baadhi ya serikali, ikiwa ni pamoja na ya Ujerumani, zinajenga uhusiano kwa siri na serikali ya Kabul.
Kwa njia hii, Urusi imechukua nafasi ya Marekani nchini Afghanistan. Sardar Rahimi, mtafiti wa mahusiano ya kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Inalco mjini Paris amesema Marekani ilijiondoa kwa hiari na pia kuwaondoa wanajeshi wake miaka minne iliyopita.
Rahimi ameiambia DW kwamba China pia inadumisha uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kisiasa na utawala wa Taliban. Amesema ingawa Beijing haijaitambua rasmi serikali ya Taliban, lakini Rais Xi Jinping alikubali barua ya utambulisho ya balozi wa Taliban mnamo Januari 2024.
Mahakama ya ICC yatoa hati ya kukamatwa viongozi wa Taliban
Urusi ni nchi ya kwanza kutambua rasmi utawala waTaliban hapo mapema mwezi Julai.
China inahitaji malighafi za Afghanistan kwa ajili ya mradi wake wa kimataifa wa miundombinu, Mpango wa ukanda wa (BRI).
Kulingana na Rahimi, nchi za Magharibi lazima zikabiliane na ukweli kwamba Taliban wanadhibiti kila nyanja ya maisha ya umma nchini Afghanistan. Amesema huu pia ndio msingi wa uhusiano kati ya nchi nyingine na utawala wa Taliban.
Waafghan wafukuzwa kutoka Ujerumani
Ujerumani imewezesha safari mbili za ndege za kuwafurusha raia wa Afghanistan tangu Taliban ilipoingia madarakani mnamo mwezi Agosti mwaka 2021. Jumla ya raia 109 wa Afghanistan walirudishwa nchini mwao na zaidi ya nusu ya watu hao walikutwa na hatia ya makosa mbalimbali. Hii inawalazimu maafisa wa Ujerumani kufanya mazungumzo ya kina na utawala huo.
Mnamo mwezi Julai, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul alithibitisha kuwa kulikuwa na mawasiliano na watawala wa Taliban katika ngazi ya kiufundi. Amesema hili ni suala la kivitendo ambalo halina athari za kisiasa au kisheria. Waziri wa Mambo ya Nje wa amesema serikali ya Ujerumani inahitaji kuwasiliana na tawala nyingi na serikali ambazo maoni na matendo yao hayalingani na ya Ujerumani kwa sababu wakati mwingine maslahi ya Ujerumani yanahitaji nchi hiyo ibaki katika mawasiliano ya aina fulani.
Pro Asyl yafungua kesi dhidi ya Wadephul na Dobrindt
Mashirika ya haki za binadamu kama lile la Pro Asyl yamekosoa safari hizo za ndege yamesema ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Mkataba wa Ulaya wa Haki za Binadamu, ambao unaambatana na mkataba wa kimataifa, unakataza kuwarudisha watu hadi kwenye nchi ambako kuna hatari ya kutendewa unyama.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema kuna ongezeko kubwa la wanaorejeshwa nchini Afghanistan na hatua hiyo inaleta changamoto kubwa kwa utawala wa Taliban, kwani wahamiaji hao wa zamani wanarejea nchini humo wakiwa hawana makazi, kipato au kazi.
UNHCR immesema, janga hili la kibinadamu linatumiwa na utawala wa Taiban wa itikadi kali kuhakikisha kuna udhibiti wa hali ya juu na kuzifedhehesha nchi za Magharibi ambazo ni lazima zitafute njia ya kuwasiliana na serikali ya Taliban.
Mashirika huru ya waangalizi yameripoti ukiukaji unaoendelea wa haki za binadamu nchini Afghanistan. Haki za wanawake hasa ndio zinatumiwa kama njia ya kupata fursa ya kufanyika mazungumzo, amesema Shukria Barakzai, mwanadiplomasia wa zamani wa Afghanistan.
Ameiambia DW kwamba wanawake wameondolewa kikamilifu kutoka kwenye maisha ya umma nchini Afghanistan tangu Taliban ilipochukua udhibiti wa mamlaka. Baadhi ya wasichana milioni 1.4 walio na umri wa miaka 12 na zaidi hawaruhusiwi tena kuhudhuria shule, na wamepigwa marufuku kuwenda kwenye shule za upili na vyuo vikuu.
UN yaitaka Taliban kuondoa vikwazo kwa wanawake Afghanistan
Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP linakadiria kuwa kila raia mmoja kati ya wanne nchini Afghanistan anakabiliwa na uhaba wa chakula, na kila mtoto kati ya watoto tatu ana utapiamlo.
Mgogoro wa kibinadamu umeongezeka wakati Marekani ilipovunja shirika la misaada la USAID, hatua ambayo imesababisha watu milioni tatu kukosa huduma za matibabu huku zahanati 420 zimefungwa nchini Afghanistan.