Je, Taifa Stars itatoboa Kombe la Dunia 2026?
8 Septemba 2025Mashabiki na wadau wa soka nchini Tanzania wameendelea kuonesha matumaini makubwa kuhusu nafasi ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kufuzu kwa mara ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Taifa Stars Jumanne itashuka Dimbani kukwaana dhidi ya Niger Mchezo wa Kuwania kufuza Kombe la Dunia 2026 mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye dimba la Amaan Complex, Zanzibar.
Wadau wa Soka Tanzania wanasema Safari ya Timu ya Taifa ya Tanzania kufuzu Kombe la Dunia ni ndefu na ngumu.
“Naona tuna nafasi Finyu kwenye kundi tayari kinara wa kundi ambaye ni Morocco ameshafuzu tunakwenda kukamilisha Ratiba na kujiweka vizuri kwenye viwango vya FIFA ”Alisema shabiki wa Taifa Stars Fred Cheti
“Mimi naona nafasi ipo kama tuna nafasi ya kucheza kwenye (best looser) na tukapata hiyo nafasi mimi naamini tunaweza tukapambana” Amesema shabiki wa Taifa Stars Ibrahim Tosha
“Uwezekano wa kutoka hapa ni asilimia kama 90 tunaweza tukatoka kutokana na aina ya Timu tulizonazo na ushindani lakini sasa ugumu utakuja kwenye mechi za mtoano” Alisema shabiki wa Taifa Stars Carlos Alexander
Tanzania haijawahi kufuzu kwa Kombe la Dunia na Hapa Mchambuzi wa Soka Johanes Michael kuhusu nafasi ya timu ya taifa katika kuwania kucheza kombe la dunia.
“Tuna ufinyu Mkubwa japokuwa ukitazama alama tulizokusanya alama 10 ni alama bora zaidi ambazo zinatuhakikishia nafasi ya pili na kucheza kama (best loser) ukitazama ushindani wa Timu ya Taifa kwenye michezo ya kufuzu kombe la Dunia tumekuwa na mwendelezo mzuri zaidi japo bado tuna kazi ngumu” amesema mchambuzi wa Soka Johanes Michael.
Tanzania ipo katika Kundi E la michuano ya Kuwania kufuza Kombe la Dunia 2026 huku Morocco Tayari wameshafuzu moja kwa moja kucheza Kombe la Dunia baada ya kujikusanyia alama 18 wakati Tanzania wamekusanya alama 10 nafasi ya pili katika kundi hilo.
Na Shamra shamra za kuanza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara zimeanza nchini Tanzania ambapo Jumatano ya Septemba 10 Simba watakwaana na Gor Mahia FC ya Kenya katika Simba Day.
“Mara hii tumejaribu kuangali nje ya Box kwa kuwa na shughuli mbalimbali ambazo zitatuweka karibu na jamii lakini Tiketi za Simba Day zitakuwa zimemalizika kwa sababu kasi ya wanasimba ni kubwa sana'' Amesema Mtendaji Mkuu wa Simba Zubeda Sakuru
Wakati huo huo Yanga watachuana na Bandari FC ya Kenya ijumaa ya Septemba 12 katika Yanga Day .
“Kenya wanawatuma Bandari Fc wanawapiga maneno sana kwamba nendeni mkawaharibe Yanga shughuli lakini sisi tunaamini Tuna Timu bora na hiyo mechi itakuwa mechi ambayo ni ya burudani na sio ya kukamian'' Amesema Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe
Yanga na Simba zinatarajia kukwaana katika Mechi ya Ngao ya Jamii ikiwa ni pambano la ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania bara mechi ambayo itachezwa Septemba 16 .