Mamlaka za Uturuki zimewakamata waandishi kadhaa wa habari kama sehemu ya shinikizo dhidi ya maandamano yaliyoibuka baada ya kumshikilia Meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu, ambaye ni mpinzani mkuu wa Rais Recep Tayyip Erdogan. Zaidi ya watu 1,000 wamekamatwa hadi sasa. Bruce Amani amezungumza na Mohammed Abdulrahman, mchambuzi wa siasa za kimataifa.