Njaa yatumika kama silaha ya vita katika maeneo ya migogoro
20 Agosti 2025Shayna Lewis, m shauri mkuu wa masuala ya Sudan wa shirika la Marekani, PAEMA amesema njaa inatumika kama silaha ya kivita alipokuwa anazungumzia juu ya hali ya nchini Sudan. Amesema sheria ya kimataifa ya kulinda haki ya binadamu inakiukwa. Lewis amesema wanaotenda maovu hayo lazima wawajibishwe.
Watoto 21 wafariki kwa utapiamlo Gaza
Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu pamoja na lile la Amnesty International yametoa kauli kama hiyo kuhusiana na hali ya Ukanda wa Gaza ambapo Israel imekuwa ikizuia chakula kuwafikia watu wa sehemu hiyo. Mshauri Shayna Lewis, amesema hatua ya kutumia njaa kama silaha ya kivita ni lazima ikomeshwe.
"Kuhisi njaa ni hisia ya asili lakini njaa kubwa inaweza kuwa ni uamuzi wa kisiasa. inaweza kutumika kama silaha ya kivita, kama ambayvo inatumika kote ulimwenguni kwa sasa. Lakini jambo hili linabidi likomeshwe. Ni kinyume cha sheria za kimataifa. Wahalifu lazima waadhibiwe.”
Afisa: Watu 63 wafariki kwa utapiamlo ndani ya wiki moja huko El-Fasher, Sudan
Shayna Lewis anazungumza juu ya hali katika mji wa El Fasher, nchini Sudan ambao umezingirwa kwa muda wa mwaka mmoja. Watu wapatao 30,000 wamenaswa. Mshauri huyo wa masuala ya haki za binadamu amesema huo ni uhalifu.
Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yamesema hali kama hiyo inatokea pia kwenye Ukanda wa Gaza. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Michael Fakhri, amesema Israel inawanyima watu chakula kwenye Ukanda wa Gaza.
Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, kumekuwapo na njaa iliyosababishwa na migogoro nchini Nigeria, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Syria na Yemen.
Kuzuiwa kwa chakula kwa makusudi kuwafikia watu ni uhalifu wa kivita.
Wataalamu wa masuala ya chakula wameeleza kwamba mashambulio ya Urusi dhidi ya sekta ya kilimo nchini Ukraine pia yanaweza kuonekana kuwa ni uhalifu wa kutumia chakula kama silaha ya kivita.
Kuzuiwa kwa chakula au vitu vingine muhimu, kwa makusudi kuwafikia watu kwa ajili ya maisha yao ni uhalifu wa kivita. Lakini mpaka sasa, wale wanaoitumia silaha hiyo bado hawajawajibishwa mahakamani. Wanaotenda uhalifu wa kivita kwa kutumia njaa hawajawahi kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa.
Guterres: Njaa haipaswi kuwa silaha ya vita
Mnamo mwaka wa 2018, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja azimio la kulaani kusababisha njaa kwa raia kuwa silaha ya kivita." Mashirika mengi ya kimataifa yameendelea kutoa miito dhidi ya kutumia njaa kama silaha ya kivita kama inavyotukia kwenye Ukanda wa Gaza.
WFP: Mamilioni ya wakimbizi wa Sudan wako hatarini kukabiliwa na njaa
Na kama inavyofahamika mahakama ya kimjataifa imetoa waranti juu ya kumkamata waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusiana na hali ya Ukanda wa Gaza. Hati hiyo imezingatiwa duniani kote katika kipindi cha muongo uliopita. Misingi yote ya sheria ipo lakini kinachokosekana ni hatua za uitekelezaji.