Je, Leverkusen itafurukuta dhidi ya Atletico Madrid?
20 Januari 2025Borussia Dortmund inayoyumba katika ligi ya nyumbani itakuwa ugenini dhidi ya Bologna, Benfica itakuwa mwenyeji wa Barcelona, AS Monaco itakutana na Aston Villa, na wawakilishi wengine wa Ujerumani Stuttgart watakipiga na Slovan Bratislava. Katika uwanja wa Anfield Liverpool inachuana na Lille.
Kazi kubwa inatarajiwa siku ya Jumatano ambapo, mabingwa wawili watakuata katika mechi ngumu, Manchester City wamechukua pointi moja pekee kutoka katika mechi zao tatu zilizopita za Ligi ya Mabingwa na wanashika nafasi ya 22 katika msimamo wa timu 36.
PSG, waliofuzu nusu fainali msimu uliopita, wako pointi moja nyuma ya City katika nafasi ya 25, eneo la hatari ikizingatiwa kwamba ni timu 24 pekee zinazofuzu kwa awamu ya muondoano.
Mechi nyengine zinazosubiriwa kwa hamu, Barcelona na Atalanta, Girona dhidi ya Arsenal, Feyenoord Rotterdam inawakaribisha Bayern München, Real Madrid itakuwa dimbani na Salzburg na AC Milan Itakuwa mwenyeji wa Girona.
Soma pia: Bayern Munich yaendeleza kujiimarisha katika Champions