Mabingwa mara moja wa Ujerumani Bayer Leverkusen wamempata kocha mpya baada ya Xabi Alonso kuihama klabu hiyo na kuelekea kujiunga na Real Madrid ya Uhispania. Erik Ten Hag ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Manchester United na Ajax Amsterdam, ndiye atakayeifunza Leverkusen sasa. Je, Ten Hag ataendesha vipi meli ya Leverkusen inayoonekana kuyumba na kuondoka kwa Alonso na wachezaji muhimu?