Ufaransa imtangaza kuwa itatambua rasmi taifa a Palestina mwezi Septemba mwaka huu. Ni hatua iliyozua hisia kali duniani: Wapo wanaoiona kama mwanga mpya wa matumaini kwa amani ya Mashariki ya Kati, na wapo wanaohofia kwamba inaweza kuchochea migawanyiko zaidi katika eneo hilo.