Japan yahimiza amri ya Trump kuhusu ushuru irekebishwe
8 Agosti 2025Matangazo
Mpatanishi mkuu wa Japan kuhusu masuala ya ushuru Ryosei Akazawa ameihimiza Marekani kudurusu upya na kurekebisha agizo la rais kuhusu ushuru katika mikutano yake na maafisa wa vyeo vya juu wa Marekani mjini Washington.
Serikali ya Japan imesema Akazawa alifanya mazungumzo jana Alhamisi na waziri wa biashara wa Marekani Howard Lutnick kwa muda wa masaa matatu na baadaye akakutana na waziri wa fedha Scott Bessent kwa dakika 30.
Ushuru wa kimataifa uliowekwa na rais wa Marekani Donald Trump ulianza kutekelezwa jana Alhamisi na kuziwacha nchi washirika zikihangaika na kufanya juhudi kupata nafuu kutokana na ongezeko la ushuru ambao unaubaili mkondo wa biashara ya kimataifa.