SiasaJapan
Japan yaandaa mkutano kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD)
20 Agosti 2025Matangazo
Wanaohudhuria Mkutano huo ni rais wa Nigeria Bola Tinubu, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, William Ruto wa Kenya na mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Japan kutoa msaada wa dola bilioni 30 kwa Afrika
Katika taarifa, ofisi ya Rais Ramaphosa imesema mgogoro wa madeni na ukosefu wa fedha katika bara la Afrika unazidisha mazingira magumu ya kijamii na kiuchumi .
Waziri mkuu wa Japan Shigeru Ishiba, amesema Japan inataka kujenga uhusiano wa kuaminiana na Afrika kwa kuzingatia mahitaji ya bara hilo.