Janga la Kibinaadamu lakaribia mashariki mwa Kongo
13 Februari 2025Matangazo
Eneo hilo tayari linawahifadhi maelfu ya watu waliokimbia vita. Gavana Jean-Jacques Purusi Sadiki ameliambia shirika la habari la Reuters akiwa mjini Bukavu kuwa kuna mmiminiko wa watu wanaokimbia Goma kuingia Kivu Kusini.
Amesema usafiri kati ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini umesitishwa, na hivyo kusababisha uhaba wa chakula. Waasi wamekuwa wakielekea Kusini tangu walipoukamata mji mkubwa wa mashariki ya Kongo, Goma mwishoni mwa mwezi Januari, na kuendelea kuyakamata maeneo zaidi, licha ya juhudi za upatanishi.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa karibu watu 3,000 wameuawa katika siku za machafuko yaliyofuatia kukamatwa kwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.