SiasaSyria
Jamii ya kimataifa yaahidi dola bilioni 6 kwa ujenzi Syria
18 Machi 2025Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa Kamishena wa Umoja wa Ulaya Dubravka Suica katika mkutano wa uchangishaji fedha uliofanyika mjini Brussels.
Soma pia: Syria yaahidi kuzuia makabiliano ya kulipa kisasi
Mawaziri wa Ujerumani, wa mambo ya kigeni Annalena Baerbock na mwenzake wa maendeleo Svenja Schulze, wametangaza yuro milioni 300 za kusaidia suala la misaada ya kiutu, mashirika ya kiraia na elimu, huku fedha hizo pia zikilenga kuwasaidia wakimbizi wa Syria na jamii zinazowahifadhi nchini Jordan, Lebanon, Irak na Uturuki.
Marekani haikutoa ahadi yoyote ya fedha ikiyataka mataifa mengine sasa kuchukua kile ilichosema ni jukumu ambalo imekuwa ikilibeba kwa miaka mingi iliyopita.