Dominika na Kenya zatoa wito wa msaada zaidi nchini Haiti
13 Mei 2025Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Dominika Roberto Alvarez na mwenzake wa Kenya Musalia Mudavadi, wametahadharisha kuwa kikosi cha kimataifa cha usaidizi wa usalama MSS nchini Haiti kinapitia changamoto kubwa katika kukabiliana na ongezeko la vurugu za magenge kutokana na uhaba wa fedhaa na msaada wa vifaa.
Soma pia: UN: Haiti huenda ikakabiliwa na ghasia zaidi
Kenya ilituma maafisa wake wa polisi kujiunga na kikosi cha kimataifa cha usaidizi wa usalama MSS mnamo mwezi Juni, mwaka jana 2024. Kikosi hicho kina takriban maafisa 1,000, ambapo karibu asilimia 75 wanatoka Kenya.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu 2025 pekee, zaidi ya watu 1, 600 wameuawa nchini Haiti na zaidi ya wengine milioni moja wamekimbia makaazi yao.