JAKARTA.´Mamia wafanya maandamano baada ya wakirsto watatu kuuwawa
22 Septemba 2006Matangazo
Mamia ya watu wamefanya maandamano mashariki mwa Indonesia kufuatia kuuwawa kwa kupigwa risasi wakirsto watatu.
Polisi imesema kuwa waandamanaji wenye hasira waliyachoma magari na vituo vya polisi katika vijiji kadhaa katika kisiwa cha Sulawesi.
Wakristo hao watatu waliuwawa kwa kupigwa risasi mapema leo baada ya kupatikana na hatia ya kuwashambulia waislamu miaka sita iliyopita.
Katika shambulio hilo waliwauwa takriban waislamu 70.
Adhabu hiyo ya kifo imelaumiwa na makao makuu ya kanisa katoliki ya Vatican pamoja mashirika ya kutetea haki za binadamu.