Jakarta: Ujerumani kuipatia rasmi Indonesia mtambo dhidi ya Tsunami.
14 Machi 2005Wiki 11 baada ya gharika iliyopita kusini mashariki ya Asia,waziri wa utafiti wa serikali kuu ya Ujerumani bibi Edelgard Bulmahn ameikabidhi rasmi serikali ya Indonesia waraka wa mtambo wa onyo la mapema dhidi ya Tsunami.Mkataba rasmi umetiwa rasmi mjini Jakarta kati ya waziri Bulmahn na waziri mwenzake wa Indonesia KUSAMAYANTO KADIMAN.Mtambo huo uliotengenzwa na kituo cha utafiti wa sayansi cha mjini Postdam ni sehemu ya msaada ulioahidiwa na serikali ya shirikisho kwa wahanga wa gharika ya tsunami.Minara ya kwanza yenye mabofu ya kupima nyendo za mawimbi baharini itasimamiwa msimu wa mapukutiko ujao katika eneo la bahari ya Hindi.Pekee nchini Indonesia gharika ya Tsumani iliangamiza maisha ya zaidi ya watu laki mbili .Kwa mujibu wa waziri wa utafiti wa serikali kuu ya Ujerumani bibi Edeklgard Bulmahn,mbali na Indonesia,Srilanka na nchi nyengine za bahari ya Hindi zimeelezea haja ya kupatiwa ufundi wa Ujerumani katika kujikinga dhidi ya gharika ya Tsunami.