JAKARTA: Mkutano wa dharura kati ya Japani na China
23 Aprili 2005Matangazo
Waziri mkuu Junichiro Koizumi wa Japani na rais Hu Jintao wa China wamekutana kwa majadiliano katika mji mkuu wa Indonesia,Jakarta.Lengo la mkutano huo uliopangwa kwa haraka ni kuuokoa uhusiano kati ya madola hayo makuu ya Asia.Viongozi hao wamehudhuria mkutano wa kilele wa madola ya Asia na Afrika nchini Indonesia,ambao uligubikwa na mgogoro wa nchi hizo mbili.Mzozo huo ulichomoza baada ya serikali ya Japani kuidhinisha vitabu vipya vya shule. China inasema vitabu hivyo vimepunguza uzito wa mateso yaliosababishwa na Wajapani wakati wa vita.Siku ya Ijumaa waziri mkuu Koizumi alipowahotubia wajumbe mkutanoni,alisisitiza "huzuni mkubwa" wa nchi yake kuhusu ukatili uliotendwa wakati wa Vita Vikuu vya Pili.