JAKARTA: Maandamano dhidi ya Marekani yaendelea
22 Mei 2005Matangazo
Waislamu nchini Indonesia kwa maelfu wamefanya maandamano ya amani mbele ya ubalozi wa Marekani katika mji mkuu,Jakarta.Wakibeba mabango ya kuipinga Marekani,kiasi ya watu 7,000 wamelalamika kuhusu dai kuwa Koran takatifu ilikufuriwa na maafisa wa Marekani.Jarida la Marekani, Newsweek katika toleo la tarehe 9 mwezi Mei,lilidai kuwa wasaili katika jela ya Marekani ya Guantanamo Bay kisiwani Cuba waliitupa chooni Koran takatifu.Ripoti hiyo ilisababisha maandamano katika nchi mbali mbali za kiislamu.Nchini Afghanistan watu 15 waliuawa katika machafuko yaliotokea wakati wa maandamano.Ingawa jumatatu iliyopita,jarida la Newsweek lilitangua ripoti yake,maandamano ya kuipinga Marekani yanaendelea.