Jaji wa mahakama ya juu ya Brazil amtia hatiani Bolsonaro
10 Septemba 2025Matangazo
Jaji wa mahakama ya juu kabisa ya Brazil Flavio Dino amepiga kura jana Jumanne kumtia hatiani rais wa zamani wa nchi hiyo Jair Bolsonaro kwa jaribio la mapinduzi ili aendelee kubaki madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2022.
Dino ameungana na jaji Alexandre de Moraes kumtia hatiani Bolsonaro.
Dino ni jaji wa pili katika jopo la majaji watano wanaotakiwa kupiga kura katika kesi hiyo, iliyositishwa muda mfupi baadaye na inatarajiwa kuanza tena hivi leo asubuhi na kura ya jaji Luiz Fux.