JAAFARI KUWA WAZIRI MKUU MPYA IRAQ
22 Februari 2005Matangazo
BAGHDAD:
Watu 4 wameuwawa na polisi 30 wamejeruhiwa katiuka shambulio la kujitoa mhanga lilolengwa katika mlolongo wa makamando wa kikosi cha polisi mjini baghdad leo hii.
Vikosi vya ulinzi vya Iraq vimekuwa mara kwa mara vikilengwa kushambuliwa na waasi wanaopiga vita uvamizi wa Marekani nchini Iraq na serikali ya mpito ya Iraq iliowekwa na Marekani.
Taarifa nyengine kutoka Baghdad inasema Umoja wa vikundi mbali mbali vya wafuasi wa madhehebu ya shiia nchini Iraq,vimemteua Bw.Ibrahim al-Jaafari kiongozi wa chama cha kiislamu cha DAWA PARTY kuwa waziri mkuu wa Iraq.
Taarifa zinasema mpinzani wake mkubwa na kipenzi cha zamani cha PENTAGON-wizara ya ulinzi ya Marekani-Ahmad Chalabi, amejitoa katika kinyan’ganyiro hiki.
.