Istaenbul: Duru rasmi zinasema Uturuki imetia saini itifaki inayopiga ...
10 Januari 2004Matangazo
marufuku adhabu ya kifo hata katika nyakati za vita.Uamuzi huo unaambatana na masharti yaliyotolewa kuweza kujiunga na Umoja wa Ulaya.Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje amesema muakilishi wa nchi yake katika baraza la Ulaya ametia saini mkataba kuhusu haki za binaadam.Kamisheni kuu ya Umoja wa Ulaya imeusifu uamuzi huo wa Uturuki na kuutaja kua hatua muhimu kuelekea demokrasia ya nchi za magharibi.Na mjini Berlin,waziri wa mambo ya nchi za nje Joschka Fischer amezisuta hoja kama Uturuki ikubaliwe uanachama na Umoja wa ulaya.Katika warsha ya kimataifa kuhusu Ulaya mjini Berlin,waziri Joschka Fischer amekumbusha Umoja wa Ulaya umeelezea uwezekano wa Uturuki kua mwanachama tangu miaka 40 iliyopita.Mwanadiplomasia ahuyo wa ujerumani ameitaka serikali ya Uturuki iendelee na utaratibu wa mageuzi.Warsha hiyo inahudhuriwa pia na waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.