Israeli kuamua kuhusu mpango wa kuudhibiti Ukanda wa Gaza
7 Agosti 2025Matangazo
Serikali ya Israel itapitisha uamuzi muhimu kuhusu mpango wa kuvitanua vita katika Ukanda wa Gaza na kulikalia kabisa kikamilifu eneo hilo la Wapalestina.
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba mkuu wa jeshi la Israel Eyal Zamir ameelezea wasiwasi wake kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakati wa mazungumzo kuhusu kuvitanua vita vya Gaza.
Zamir ametahadharisha kwamba hatua ya kuukalia ukanda wa Gaza huenda ikawa kama kujiingiza katika mtego na kukasababisha athari na kuwaumiza mateka waliosalia.