Israel yawauwa wafanyakazi 15 wa afya Gaza
1 Aprili 2025Matangazo
Miili hiyo iligunduliwa imezikwa na magari yao ya wagonjwa kwenye kaburi la pamoja linaloshukiwa kuchimbwa na matingatinga ya jeshi la Israel.
Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina linasema wafanyakazi wake hao na magari yao walikuwa na alama za wazi kuwa ni huduma za kiafya na kibinaadamu na inawatuhumu wanajeshi wa Israel kwa kuwauwa kwa makusudi.
Israel inadai kuwa wanajeshi wake walizifyatulia risasi gari ambazo zilikuwa zinawakaribia zikiwa hazina alama yoyote.
Miili hiyo ni ya wafanyakazi wanane wa Hilali Nyekundu, sita wa huduma za dharura na mmoja wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNRWA.