MigogoroIsrael
Israel yawashambulia wapiganaji wanaowalenga jamii ya Druze
1 Mei 2025Matangazo
Israel inafanya shambulizi hilo huku mapigano katika viunga vya kusini mwa Damascus yakiendelea.
Shirika linalofuatilia vita nchini Syria la Syrian Observatory for Human Rights, limesema mapigano yalikuwa "kati ya makundi ya wenyeji waliokuwa na silaha kutoka jamii ya Druze na vikosi vyenye ushirikiano na wizara za ulinzi na mambo ya ndani na vikosi vingine vya kiwakala."
Tangu kuangushwa kwa Rais Bashar Assad wa Syria, Disemba mwaka uliopita, Israel imepeleka wanajeshi wake kusini mwa Syria. Na kulingana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, "Israel haitaruhusu madhara kwa jamii ya Druze nchini Syria kutokana na msaada wao mkubwa nchini Israel na ambao wameunganishwa kihistoria.