Israel yalaani shambulizi dhidi ya wafanyakazi wake
22 Mei 2025Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Gideon Saar,amewalaumu baadhi ya viongozi wa Ulaya,akisema wanawajibika kwa mauaji ya wafanyakazi wawili wa ubalozi wa nchi hiyo waliopigwa risasi huko Washington,Marekani.
Akizungumza na waandishi habari leo hukoJerusalem,Saar amesema kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya chuki dhidi ya wayahudi na kauli za chuki dhidi ya Israel ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi na maafisa wa mataifa mengi na hasa barani Ulaya, ikiwemo mashirika ya Kimataifa.
Waziri mkuu BenjaminNetanyahuambaye ametoa mwito wa kuimarishwa usalama kwenye balozi zote za nchi yake duniani, amesema ametamaushwa na mauaji hayo ya kutisha yaliyosababishwa na chuki dhidi ya wayahudi. Viongozi mbali mbali wa dunia wamelaani tukio hilo la Washington.