Israel yaushambulia mji wa Homs nchini Syria
9 Septemba 2025Matangazo
Mashambulizi ya kutokea angani ya Israel yameyalenga maeneo ya katikati na magharibi mwa miji ya Syria ya Homs na Latakia Jumatatu jioni.
Taarifa hiyo imeripotiwa na shirika la habari la serikali ya Syria, SANA.
Shirika linalofuatilia masuala ya haki za binadamu la Syria lenye makao yake jijini London nchini Uingereza limeripoti kwamba mashambulizi ya Israel karibu na Homs yalilenga kambi ya jeshi kusini mwa mji huo.
Israel haijathibitisha shambulizi hilo lakini waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Israel Katz amesema vikosi vinafanya operesheni mchana na usiku kila inapohitajika kwa usalama wa nchi.