Israel yatoa amri kwa wapalestina kuondoka Gaza
20 Julai 2025Matangazo
Msemaji wa jeshi hilo Avichay Adraee ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba wakaazi na watu waliopoteza makao wanaohifadhiwa katika eneo la Deir el-Balah wanapaswa kuondoka mara moja.
Amewataka Wapalestina kuelekea maeneo ya Kusini katika eneo la Al Mawasi katika pwani ya Mediterenia.
Watu 26 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel
Idadi kubwa ya idadi jumla ya watu wa Gaza wapatao milioni mbili wamepoteza makaazi yao katika vita hivyo vilivyoingia mwezi wake wa 22.
Awali Shirika la Uratibu wa Masuala ya Kiutu ya Umoja wa Mataifa-Ocha lilisema mwezi Januari kwamba asilimia 80 ya watu katika ukanda wa Gaza wamekuwa wakitatizwa na ameri ya kuondoka waliko kutoka kwa serikali ya Israel.