Israel yathibitisha kupokea mwili wa mateka Shiri Bibas
22 Februari 2025Matangazo
Siku ya Ijumaa, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliilaumu Hamas kwa kushindwa kukabidhi mwili wa mama huyo wa watoto wawili aliyetekwa nyara na kundi hilo na kuahidi kuchukua hatua kali.
Hamas yachunguza kosa katika kutambua mwili wa Shiri Bibas
Leo hii, Hamas imewaachia huru mateka sita wa Israel na kuwakabidhi kwa maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu. Mabadilishano hayo ya mateka na wafungwa ni sehemu ya makubaliano ya usitishwaji mapigano huko Gaza.