Israel yathibitisha kumuua afisa wa Hezbollah mjini Beirut
1 Aprili 2025Matangazo
Israel imethibitisha imemlenga na kumuua afisa wa kundi la Hezbollah Hassan Ali Badir katika shambulizi la usiku wa kumkia leo mjini Beirut.
Watu wanne wameuwawa katika shambulizi hilo ambalo lilifanywa bila tahadhari wakati wa sikukuu ya Eid al-Fitr kusherehekea mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Wizara ya afya ya Lebanon imethibitisha kuuwawa kwa watu watatu na imesema wengine saba wamejeruhiwa.
Waziri mkuu wa Lebanon Nawaf Salaam amesema shambulizi hilo ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya usitishaji mapigano ambayo kwa kiasi kikubwa yalifikisha mwisho kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja wa uhasama kati ya Israel na Hezbollah.