Israel yatangaza kutanua mashambulizi Ukanda wa Gaza
12 Aprili 2025Ametoa tangazo hilo wakati jeshi la Israel likidai kuwa limeuzingira mji wote wa Rafah kusini mwa ukanda huo. Jeshi hilo limesema pia kuwa limeanzisha ukanda mpya wa usalama wa Morag ndani ya Ukanda wa Gaza.
Soma zaidi: Israel yasema jeshi lake linapanua operesheni zake Gaza
Ukanda huo wa Morag sasa unaitenganisha miji ya Rafah na Khan Younis. Sambamba na njia ya Netzarim inayodhibitiwa pia na Israel, sasa Ukanda wa Gaza umegawanyika katika sehemu tatu. Waziri wa Ulinzi wa Israel Katz, ameelezea hatua ya kuyadhibiti maeneo hayo kuwa kanda za usalama zinazokusudiwa kutumiwa kwa maslahi ya Israel.
Wakati huohuo jeshi la Israel limewataka wakaazi wengi wa mji wa Khan Younis kabla ya mashambulizi linalopanga kuyafanya. Hatua hiyo imetangazwa baada ya kombora kurushwa kuelekea Israel kutoka Kusini mwa Gaza.