Israel yataka mateka wote 50 waachiwe huru
19 Agosti 2025Matangazo
Afisa huyo ambaye hakutaka kutajwa jina, amesema msimamo wa serikali ya Israel haujabadilika na inataka mateka wote waachiwe huru.
Israel imeelezea hatua hiyo siku moja baada ya kundi la wanamgambo la Hamas kulikubali pendekezo jipya la kusitisha mapigano Gaza.
Aidha, shirika la utangazaji la Israel, Kan, limevinukuu vyanzo vya ofisi ya Waziri Mkuu vikizungumzia taarifa hiyo.
Israel imetangaza msimamo wake wakati mazungumzo kuhusu makubaliano yaliyopendekezwa ya kusitisha mapigano kwa siku 60 na kuachiliwa kwa nusu ya mateka yakiwa yanaendelea.