Israel yataka kilio cha mateka kiwe ajenda ya kimataifa
4 Agosti 2025Video hizo zilizidisha hofu juu ya maisha ya mateka hao baada ya karibu miezi 22 kifungoni.
Waziri wa Mambo ya kigeni wa Israel, Gideon Saar amewaambia waandishi wa habari kabla ya mkutano wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na suala hilo, akiutaka ulimwengu kukomesha hali ya utekaji nyara wa raia.
"Jamii ya Kimataifa inapaswa kuzuia jambo hili lisiwanufaishe magaidi. Ulimwengu unatakiwa kukomesha hali ya utekaji wa raia. Na ndio maana ninakwenda New York leo kushiriki kikao nilichokiomba cha Baraza la Usalama kinachofanyika kesho kuhusu suala la mateka. Ninashukuru Marekani na Panama kwa kuitikia wito wetu na kusaidia mkutano huu muhimu na wa dharura kufanyika."
Kikao hicho kimeitishwa baada ya Hamas na mshirika wake Islamic Jihad kuchapisha wiki iliyopita video tatu zinazoonyesha mateka Rom Braslavski na Evyatar David wakiwa dhaifu na kusababisha mshtuko mkubwa nchini Israel.
Miongoni mwa mateka 251 waliochukuliwa na Hamas wakati wa shambulizi la Oktoba 2023 nchini Israel, 49 bado wanazuiliwa Ukanda wa Gaza.